MAULID NA KUMHESHIMU NA KUMTUKUZA BWANA MTUME (S.A.W.W.):
Katika Qur'ani Tukufu (Sura 7:157), Mwenyezi Mungu anawasifu, na kuwaita "wenye kufaulu", wale ambao humtukuza na kumheshimu Mtume Wake (s.a.w.w.), wakamsaidia na kuyafuata yale aliyoyaleta.
Lakini tutawezaje kuyafanya hayo kama mtu mwenyewe hatumjui vilivyo?
Waswahili husema: "Jambo usilolijua ni usiku wa kiza"; na "asiyekujua hakuthamini". Kwa hivyo, bila ya kumjua Mtume (s.a.w.w.) vilivyo -- historia yake, sifa zake, cheo chake, utukufu wake, na kadhaalika -- vipi tutaweza kumthamini na kumtukuza?
Ndipo wanazuoni, kwa kuwa si kila mtu aweza kusoma vitabu, wakabuni maulidi ili yawe ni chombo cha kumjulisha Bwana Mtume (s.a.w.w.) apate kuheshimiwa na kutukuzwa.
Hivyo katika maulidi, watu hupata fursa ya kuelezwa yote ya Mtume (s.a.w.w.). Na kwa kuyajua hayo, watu humpenda; na kama ilivyo desturi ya kila apendaye kumfuata yule anayempenda, watu humfuata.
Jee, kama maulidi yanasaidia watu kumjua Mtume (s.a.w.w.), kumkumbuka na kumpenda, huoni kuwa tunatekeleza maagizo ya Mtume hapo?
Kama wewe hupendi kumsifu na kutangaza Mtume, kaa kimya tuachie sisi tufanye kazi.
Comments
Post a Comment