MAULID NA USOMAJI WA QUR’AN
Kwa kuwa Maulid ni ibada inayoambatana na Usomaji wa Qur’an, bila shaka
wasoma maulid hupata thawabu nyingi sana.
Qur'ani (k.m. Sura 73:4 na 20), tunaona jinsi
Mwenyezi Mungu anavyotuamrisha tuisome. Na tunapokuja kwenye Hadithi zake,
tunaelezwa kwamba Bwana Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda sana mtu amsomee yeye
Qur'ani, na yeye akisikiliza.
Jee, pale tunapoyafungua maulidi yetu kwa
mmoja wetu kuisoma Qur'ani, na wengine tukawa tunamsikiliza, huwa -- kama
hatukufanya la sunna?
Hakika tunaposoma Qur’an katika maulid huwa
tumefanya sunnah ya mtume kiasi kwamba hustahili kulipwa malipo makubwa toka
kwa Muuma wetu.
Comments
Post a Comment