MAULID NA USOMAJI WA QUR’AN

MAULID NA USOMAJI WA QUR’AN
Kwa kuwa Maulid ni ibada inayoambatana na Usomaji wa Qur’an, bila shaka wasoma maulid hupata thawabu nyingi sana.
Qur'ani (k.m. Sura 73:4 na 20), tunaona jinsi Mwenyezi Mungu anavyotuamrisha tuisome. Na tunapokuja kwenye Hadithi zake, tunaelezwa kwamba Bwana Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda sana mtu amsomee yeye Qur'ani, na yeye akisikiliza.
Jee, pale tunapoyafungua maulidi yetu kwa mmoja wetu kuisoma Qur'ani, na wengine tukawa tunamsikiliza, huwa -- kama hatukufanya la sunna?
Hakika tunaposoma Qur’an katika maulid huwa tumefanya sunnah ya mtume kiasi kwamba hustahili kulipwa malipo makubwa toka kwa Muuma wetu.

Comments