HAKI YA URAFIKI
Mji wa Kufa ulikuwa Makao makuu
na kituo cha serikali ya kiislamu. Macho yote ya umma wa Kiislamu (isipokuwa
Sham) yalikuwa yanaangalia mji huu huku yakisubiri ni amri gani zinazotolewa na
uamuzi gani unaochukuliwa.
Nje ya mji, mabwana wawili
mmoja Mwislamu na mwingine hakuwa mwislamu, walikutana njiani siku moja.
Mwislamu alikuwa akielekea mji wa Kufa na yule bwana mwingine akielekea
kwingine karibu na mji wa Kufa. Kwa kuwa sehemu fulani ya safari yao ilikuwa ni
moja waliamua kutembea pamoja.
Walipokuwa njiani walizungumza
kiasi kuhusu mambo yaliyowahusu hadi walipofika sehemu njia zao zinapoachana.
Bwana yule ambaye si Mwislamu alishangaa kuona rafiki Mwislamu hakuendelea na
safari yake kuelekea Kufa bali aliendelea kumshindikiza alikokuwa akilekea.
Akamuuliza: “Haya, si
ulinieleza kuwa ulikuwa unakwenda Kufa?” “ Ndio.”
“Basi kwa nini unapita njia
hii? Hiyo njia nyingine ndio ya Kufa”
“Najua, nataka nikushindikize
kidogo ili nikuage. Kwa sababu Mtume wetu (s.a.w.w) amesema, ‘Wakati wowote
watu wawili wanapotembea pamoja wanaanzisha haki baina yao.’ Sasa hivi una haki
juu yangu na kwa sababu hiyo ningependa kutembea hatua kadha na wewe kisha
baadaye nirudi kwenye njia yangu.”
Yule mtu alisema, “Oh! Mamlaka
na madaraka yaliyotawala miongoni mwa watu katika njia kamilifu kutoka kwa
Mtume wenu, na kasi ya kushangaza ya kuenea dini yake dunia nzima, nina hakika
lazima iwe ni kwa sababu ya tabia yake ya kiungwana.”
Kushangaa na kuvutiwa kwa bwana
huyu kulifikia kileleni pale alipogundua baadaye kuwa yule rafiki yake Mwislamu
alikuwa Ali bin Abi Talib (a.s) ambaye alikuwa Khalifa wa wakati huo. Muda
mfupi baadaye alisilimu na akawa miongoni mwa wafuasi wa dhati na mwenye
kujitolea muhanga wa Ali (a.s).
Comments
Post a Comment