KUFUNGA MIKONO KATIKA SWALA NI KITENDO CHA MAJUSI

KUFUNGA MIKONO KATIKA SWALA NI KITENDO CHA MAJUSI
Baada ya kuthibitisha kuwa hakuna hadith sahihi inayosema kuwa kufunga mikono katika swala ni wajibu au sunnah.
Jifunze swala sahihi toka kwa Maimamu Watukufu wa Ahlul-bayt (a.s) - wenye kujua sunna za Mtume (s.a.w.w) zaidi na wenye elimu zaidi ya mtu yeyote yule.
Wao walikuwa wakijiepusha na kitendo hicho cha kufunga mikono katika swala na kukiona kuwa ni kitendo cha " Majusi, hawa ndio waliokuwa wakikitenda mbele ya mfalme"!.
Zuraara amepokea kutoka kwa Abi Jaafar (a.s) kwamba amesema:
(( وعليک بالإقبال علی صلاتک ، ولا تکفِّر ، فإنما يصنع ذلک المجوس))
"Inatakiwa uitilie umuhimu swala yako (uiswali kwa umakini zaidi), na usifunge mikono, kwani anayefanya hivyo ni Majusi"
((Na Swaduq amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Imam Ali (a.s) kwamba amesema:
(( لا يجمع المسلم يديه في صلاته وهو قائم بين يدي الله عز وجل يتشبه بأهل الکفر- يعني المجوس-))
((Muislaam asikusanye (asifunge) mikono yake katika swala yake huku akiwa amesimama mbele ya Allah (s.w), (kwani akifanya hivyo) anajifananisha na makafiri-yaani Majusi-)).
((Tazama hadithi hii katika kitabu kiitwacho: Wasaailu (cha Hurru Al-a'miliyyu) : Juzu ya 4, Mlango wa 15 katika Milango inayozungumzia vibatilishi vya swala")).
FAHAMU KWAMBA: Hii ni kauli ya Imam Ali (a.s) Imam wa Mashariki na Magharibi, tofauti na Mtume (s.a.w.w), hakuna Mwislaam yeyote (sawa sawa iwe zama hizi au zama zile za Maswahaba) ambaye anaujua Uislaam zaidi na mwenye Elimu zaidi na Mchamungu zaidi na Mwenye kumjua Mwenyeezi Mungu (s.w) na Mtume (s.a.w.w) zaidi, na Mwenye kujua sunna za Mtume (s.a.w.w) zaidi, kama Imam Ali (a.s).!
Imam Ali (a.s) anasema kufunga mikono ni kitendo cha Majusi na kufanya hivyo ni kujifananisha na Majusi, ingelikuwa Jambo hilo ni Sunna ya Mtume (s.a.w.w), basi Imam Ali (a.s) bila shaka angelitambua hilo na asingelikataza na yeye mwenyewe zingepokelewa riwaya zikisema ameonekana akiswali hivyo !!
Maana ikiwa Musa bin Umayri anasema kamuona Alqama anaswali kwa kufunga mikono, basi zingelikuwepo pia hadithi zinazosema kwamba Imam Ali (a.s) siku moja kaonekana naye akitenda sunna hiyo katika swala, maana huwezi kuniambia kauli yako ikaniingia akilini kwamba Alqama haiwezekani akaijua vizuri sunna hiyo kuliko Imam Ali (a.s)!!

Comments