KUSHEREHEKEA MAULID HUTOKANA NA KUMPENDA MTUME (S.A.W.W.)

KUSHEREHEKEA MAULID HUTOKANA NA KUMPENDA MTUME (S.A.W.W.):
Hadithi zake Mtume (s.a.w.w.) zatuhimiza tumpende, bali zinatueleza waziwazi kwamba hatuwi ni waumini mpaka tumpende yeye kuliko nafsi zetu, kuliko mali yetu na ahli zetu, bali kuliko watu wote.
Jee sifa zote zile anazosifiwa Mtume (s.a.w.w.) maulidini, furaha zote na nderemo zinazoonyeshwa maulidini, haziwi ni ushahidi wa mapenzi yetu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)? Mambo kama hayo hufanyiwa asiyependwa?
Kama kuonyesha mapenzi yetu kwa Mtume wetu ni bid'a, sunna ni ipi?
Hatuwezi kuomba radhi kwa maadui wa uislamu wanaotuzuia kumpenda Mtume wetu kwa kisingizio cha bid’a.Wao ndio wafanya bida' wakubwa.

Comments