KWA NINI MASUNNI WAMETOFAUTINA KUNYOOSHA AU KUFUNGA MIKONO KATIKA SWALA?
Ibnu Rushdi amesema: Na sababu ya kutofautiana kwao ni kwamba zimekuja riwaya thabiti ambazo zilinukuu wasifu wa Swala ya Mtume (s.a.w.w), lakini haijanukuliwa kuwa alikuwa akiweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto" (Tazama: Bidayatul-Mujtahid).
Hii ni dhahili kuwa wale wanaowafundisha watu kufunga mikono wanatapatapa na ndio maana hawana kauli moja, wengine wanasema juu ya kitovu, wengine chini ya kitovu, wengine kifuani. Kama kweli Mtume alifanya hivyo je alitofautisha kama wao, yaani leo anaweka chini ya kitovu kesho anaweka shingoni, kisha anamwambia mke wake weka kifuani. Haiwezekani, huu ni ubabaishaji wa watu hawa waliozoea kumzulia Mtume (s.a.w.w).
Wafuasi wa Malik hawafungi mikono na Imam wao (Malik) alikataa Suala hilo. Imam Maalik anasema katika kitabu chake cha Al-Mudawanaati akikataa kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto ndani ya Swala: "Silijui jambo hilo ndani Swala ya faradhi".
Hii ndio Fat-wa yake Malik na ile riwaya ya kufunga mikono katika swala aliyoipokea katika kitabu chake cha Riwaya kiitwacho: Al-Muwatta, kupokea kwake riwaya hiyo haimaanishi kwamba hiyo ni Fat'wa yake, kwani inajuzu na si jambo la ajabu mtu ukapokea riwaya na ukaipinga kulingana na ulivyoielewa na ulivyo zielewa riwaya nyingine zinazopinga jambo la kufumga mikono katika swala. Na hivi ndivyo alivyofanya Imam Maalik.
Comments
Post a Comment