MAULID HUAMBATANA NA KUTOLEANA WAADHI:

MAULID HUAMBATANA NA KUTOLEANA WAADHI:
Katika Qur'ani Tukufu (Sura 16:125) Mwenyezi Mungu anatuamrisha tulinganiane kwa hekima na mawaidha mema. Na vivyo hivyo ndivyo Bwana Mtume (s.a.w.w.) anavyotuhimiza katika Hadithi zake nyingi.
Jee, maulidini hatutoleani mawaidha na kulinganiana mema?
Bila shaka kwa kufanya hivyo hutekeleza amri Allah na Sunnah za Mtume wake (s.a.w.w)
Suala la kuambrishana kutenda mema na kukatazana kufanya maovu ni amri ya Allah (s.w). Hivyo, Maulid inatumika katika kutekelezea amri za Allah (s.w).
Wal-Hamdulillah, tuendelee kutekeleza ibada hii muhimu.

Comments