KUZALIWA KWA ALI IBN ABI
TALIB
Assalaam alaykum:
Imam Ali (a.s) alizaliwa
tarehe 13 Rajab ya mwaka wa thelathini wa Tembo (A.D. 600). Binamu yake, Mtume Muhammad
(s.a.w.w), alikuwa ana miaka thelathini wakati huo. Wazazi wa Ali walikuwa ni
Abu Talib Ibn Abdul Muttalib, na Fatima, binti Asad, wote wa ukoo wa Bani
Hashim.
Ali alizaliwa ndani ya
Al-Kaaba huko Makka. Mwanahistoria maarufu, Masud, anaandika kwenye ukurasa wa
76 wa juzuu ya 2 ya kitabu chake, Murujudh- Dhahab kwamba moja ya ubora ambao
Ali alikuwa nao ulikuwa kwamba alizaliwa ndani ya Nyumba ya Allah (s.w.t.).
Baadhi ya mabingwa wengine ambao wathibitisha
kuzaliwa kwa Ali ndani ya Al-Kaaba, ni :-
1. Muhammad Ibn Talha Shafii
katika Matalibul-usul uk 11.
2. Hakim katika Mustadrak,
uk. 483, Juz. 111.
3. Al- Umari katika Sharh
Ainia uk. 15.
4. Halabi katika Sira, uk.
165, Juz. 1.
5. Sibt Ibnul- Jauzi katika
Tadhkira Khawaisil Umma, uk.7.
6. Ibn Sabagh Malik katika
Fusuulul Muhimma uk.14
7. Muhammad Ibn Yusuf
Shafi’i katika Kifayatut-Talib uk. 261. 8. Shablanji katika Nurul Absar, uk.
76.
9. Ibn Zahra katika
Ghiyathul Ikhtisar, uk.97.
10. Edvi katika Nafahatul
Qudsia uk. 41.
Miongoni mwa wanahistoria wa
kisasa, Abbas Mahmud al-Akkad wa Misri anaandika katika kitabu chake
Al-Abqariyat ul-Imam Ali, (Cairo, 1970) kwamba Ali Ibn Abi Talib alizaliwa
ndani ya Al-Kaaba.
Mwanahistoria mwingine wa
sasa, Mahmud Said at-Tantawi, wa Supreme council of Islamic Affairs (Baraza la
juu la Mashauri ya Kiislamu), Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, anaandika katika
ukurasa wa 186 wa kitabu chake kiitwacho Min Fadha-il al-Ashrat al- Mubashirina
bil- Janna, kilichochapishwa mwaka 1976 na Matab’a al-Ahram at-Tijariyya,
Cairo, Misri hivi:- “Rehma za Allah (s.w.t.) ziwe juu ya Ali Ibn Abi Talib.
Alizaliwa ndani ya Al-Kaaba. Alishuhudia kuchipuka kwa Uislamu; alishuhudia
Da’wa ya Muhammad na alikuwa ni shahidi wa Wahyi (kushuka kwa Qur’an al-Majid).
Mara moja tu aliukubali Uislamu ingawa alikuwa bado mtoto, na alipigana maisha
yake yote ili kwamba Neno la Mungu liwe juu kabisa.”
Mshairi wa Kiarabu alitunga
ubeti ufuatao juu ya kuzaliwa kwa Ali: Yeye (Ali) ndiye yule ambaye ile Nyumba
ya Allah (s.w.t.), iligeuzwa kuwa wodi ya wazazi; Na yeye ndiye aliyeyatupa
masanamu nje ya Nyumba hiyo; Ali alikuwa mtoto wa kwanza na wa mwisho, daima
kuzaliwa ndani ya Al-Kaaba.
Ilikuwa ni desturi ya
Waarabu kwamba wakati mtoto anapozaliwa, aliwekwa chini ya miguu ya sanamu au
masanamu ya ukoo huo, hivyo kuashiria “kumkabidhi” kwa huyo mungu wa kipagani.
Watoto wote wa Kiarabu “walitolewa” kwa masanamu isipokuwa Ali Ibn Abu Talib.
Wakati watoto wengine wa Kiarabu walipozaliwa, mmoja wa waabudu sanamu alikuja
kuwasalimia na kuwabeba mikononi mwake.
Lakini Ali alipozaliwa,
Muhammad, mjumbe wa Allah (s.w.t.) alikuja kwenye eneo la Al-Kaaba kumsalimia.
Alimbeba mtoto huyo mikononi mwake, na kumtoa kwenye kumtumikia Allah (s.w.t.).
Mtume lazima awe
alikwishajua kwamba yule mtoto aliyekuwa mikononi mwake siku moja atakujakuwa
adui asiyeshindika wa wanaoabudu masanamu wote na washirikina na wa miungu yao
na miungu ya kike. Wakati Ali alipokua, aling’oa uabudu masanamu na ushirikina
kutoka Arabia kwa upanga wake.
Kuzaliwa ndani ya Al-Kaaba
kulikuwa ni moja kati ya sifa nyingi ambazo Mungu amezijaalia juu ya Ali. Sifa
nyingine aliyokuwa nayo ni kwamba kamwe hakuabudu masanamu. Hii nayo inamfanya
awe wa kipekee kwa vile Waarabu wote waliabudu masanamu kwa miaka na miaka
kabla ya kukana uabudu masanamu na kuukubali Uislamu. Ni kwa sababu hii ambapo
anaitwa, “Karama llahu waj-hahu” (“Ambaye Allah (s.w.t.) ameutukuza uso wake.”).
Uso wake ulitukuzwa hasa na
Allah (s.w.t.) kwani ulikuwa ndio uso pekee katika maswahaba ambao kamwe
haukuinama mbele ya Sanamu lolote.
Ali alikuwa ndiye mtoto
mdogo kabisa katika familia hiyo. Kati ya kaka zake watatu, Talib na Aqil,
walikuwa wakubwa kwa miaka kumi zaidi yake.
Kuzaliwa kwa Ali kuliujaza
moyo wa nabii furaha isiyo kifani. Mtoto huyu alikuwa ni mtu mmoja “maalum”
kwake yeye. Ingawaje Muhammad alikuwa na binamu wengi wengine na walikuwa na
watoto wao mwenyewe, na Ali mwenyewe alikuwa na kaka zake wakubwa watatu;
lakini hakuonyesha mvuto wowote juu ya yeyote kati yao.
Ali, na Ali peke yake ndiye
alikuwa kitovu cha mvuto wake na mapenzi.
Wakati Ali alipokuwa na
miaka mitano, Muhammad alimchukua kama mtoto wake wa kupanga, na kuanzia hapo
tena hawakutengana tena daima.
Comments
Post a Comment