MIRZA JAWAD AGHA MALIKI

MIRZA JAWAD AGHA MALIKI

Juu ya mwanazuoni Mirza Jawad Agha Maliki (aliyekufa mwaka 1343A.H.), imerekodiwa kwamba katika hatua za awali za kutafuta utakaso wa kiroho na baada ya kuwa amesoma chini ya mwalimu wake, mwanazuoni mkubwa Mulla Hasainquli Hamadani (aliyekufa mwaka 1311A.H.), kwa miaka miwili mfululizo, alikuwa akilalamika kwa mwalimu wake? “Katika kutafuta kwangu utakaso wa kiroho, bado sijaweza kupata kitu chochote”.

“Jina lako ni nani?” aliuliza mwalimu. Akajibu “Wewe hunitambui mimi? Mimi ni Jawad Maliki Tabrizi.”
Hasainquli Hamadani aliuliza, “Je una uhusiano na familia fulani na familia ya Maliki?” Mirza Jawad alikubali na kisha akaanza kuzungumza kwa kuwakosoa.

“Wakati wowote utakapofika wa wewe kuwawekea viatu vyao mbele yao ili wavae, (ambacho unakiona ni kitendo duni na dhalili), mimi binafsi nitakuja kukuongoza,” alishauri Husainquli Hamadani.

Siku iliyofuata Mirza Jawad alipokwenda darasani, alikaa nyuma ya wanafunzi wote na pole pole alianza kuzoea na kuwa na tabia ya kirafiki na wanafunzi wa familia ya Maliki wanaoishi Najaf. Iliendelea hivi mpaka ikafikia hatua ambapo alikuwa hata akiwawekea viatu mbele yao ili wavae.

Ndugu wanaoishi Tibrizi walipolijua hili, chuki na faraka iliyokuwepo miongoni mwa wanafamilia hao, na amani ikaanzishwa miongoni mwao.

Baadaye Mirza Jawad alimwendea mwalimu wake, ambaye alimwambia, “Hakuna maelekezo mapya kwa ajili yako (Baada ya kuwasuluhisha wana ndugu wa familia ya Maliki). Endelea kufuata utaratibu huu wa sheria na nufaika kutokana nayo.

Polepole Mirza aliendelea katika utafutaji wake. Alikuja katika Hauza ya Qum ambapo alianza kuwafundisha na kuwaongoza wanafunzi katika fani ya utakaso wa kiroho. Idadi kubwa ya watu wa kawaida na wasomi walinufaika kutokana naye na mafundisho yake.


Huu ndio Uislamu, upendo kwa wanadamu na kuondoa chuki baina ya watu ili watu waishi kwa amani na upendo.

Comments