HALI YA FEDHEHA NA AIBU YA JU’DAH

HALI YA FEDHEHA NA AIBU YA JU’DAH
Imamu Hasan (a.s) alikuwa mwenye sura ya kupendeza, mwenye uvumilivu mkubwa na mkarimu, na alikuwa mpole na mwenye moyo wa mapenzi kwa jamaa wa familia yake.
Baada ya kuuawa shahidi kwa Imamu Ali (as), kwa muda wa miaka kumi Mua’wiyah, alianzisha mahubiri ya chuki, udanganyifu na uadui kuhusiana na Imamu Hasan (as).
Alikusudia kumdhuru Imamu (as) katika nyakati mbalimbali, lakini hakufanikiwa kitu chochote. Kwa hiyo aliamua kumtumia mke wa Imamu Ju’dah, bint wa Asha’th Ibn Qais, ili ampe sumu.
Mua’wiyah alimshawishi kwa kumuahidi kwamba kama akimpa sumu Imamu Hasan Ibn Ali (a.s), atampa dirham elfu mia moja, na kwa nyongeza, atamuozesha kwa mtoto wake Yazid. Kwa matumaini ya kupata mali na msukumo wa kuwa mke wa Yazid, Ju’dah alikubali kutekeleza ombi lake. Mua’wiyah alimpa sumu ambayo aliipata kutoka kwa mfalme wa Urumi.
Siku ya joto kali sana, Imamu Hasan (as) alifunga (saumu). Wakati wa kufuturu, Imamu alikuwa na kiu kali mno, Ju’dah alimletea maziwa ambayo ameyachanganya na sumu.
Mara tu Imamu alipokunywa maziwa yale, alihisi athari ya sumu. Alitambua kilichotokea na akaguta kwa sauti: Inna lillahi wa inna ilaihi raajiu’n.
Baada ya kumshukuru Mungu kwamba sasa ataondoka na kutoka kwenye ulimwenu huu wa mpito kwenda kwenye ulimwengu wa milele, alimgeukia Ju’dah na akasema: “Ewe adui wa Mwenyezi Mungu! Umeniuwa, Mungu naakuuwe wewe! Kwa jina la Mungu, hutakuja pata hata kitu kidogo ambacho kwamba unakitagemea na kukitamani. Mtu yule amekudanganya. Mungu akufedheheshe wewe na yeye pia kwa njia za adhabu Zake.”
Uvumilivu wa Imamu Hasan (as) unaweza kupimwa kutokana na ukweli kwamba wakati Imamu Husein (as) alipotaka kujua jina la muuaji wake, Imamu Hasan (as) alikataa kufichua jina la Ju’dah.
Kwa mujibu wa hadithi moja, kwa siku mbili (na kwa mujibu wa nyingine, kwa siku arobaini), Imamu aliteseka kutokana na athari mbaya za sumu ile, mpaka hatimaye tarehe 28 Safar, 50 A.H., aliuaga ulimwengu huu yakinifu akiwa na umri wa miaka 48.
Amma kwa Ju’dah alibeba matumaini yake na matamanio yake hadi kwenye kaburi lake kwani Mua’wiyah alihoji kwamba kama hakuweza kuwa muaminifu kwa Hasan Ibn Ali (as), vipi atategemewa kuwa muaminifu kwa Yazid; na hivyo alikataa kutekeleza chochote katika ahadi zake.
Na kwa hali hiyo, alikufa katika hali ya fedheha na aibu.
Rejea:
Muntahal Aa’maal, Jz. 1, uk. 231.

Comments