KHALID BIN WALID (r.a)(Saifullahil-masulul)

KHALID BIN WALID (r.a)(Saifullahil-masulul)
___________________________________________
Moja wapo ya vitu mashia wanavyopondwa ,kushambuliwa na kuumbuliwa navyo pengine hata kutolewa katika uislamu ni jambo la kutukana Maswahaba wa Mtume(s.a.w.w).
Jambo linalotakiwa wajue wale wanao washutumu na kuwatuhumu Mashia kwa madai ya kuwatukana maswahaba ni kwamba mashia hawamini wala kuitakidi kuwa maswahaba wote ni waadilifu. Kwa imani yao hiyo wanaamini kuna maswahaba wema na waovu na inabidi kwa muislamu awachunguze wote ili ajue ni yupi mwema na yupi ni muovu .
Na katika hali ya kuchunguza mtu huyaona makundi hayo mawili na akitoa jawabu kusema swahaba fulani ni hivi wengine humchukulia vibaya na kuanza kusema anatukana maswahaba wa mtume na hata kama maneno yale anayosema amenukuu kutoka katika vitaba vya masunni .
Tuchukue mfano Swahaba KHALID BIN WALID (r.a)(Saifullahil-masulul) na baadhi ya mambo alio yafanya katika uhai wake kutoka kwenye vitabu vya kisuni.
Mtume(s.a.w.w) alighabishwa na kukasirishwa na Khalid bin Walid alipomtuma kwenda kwa kabila la Banii Juzaimah kwenda kuwalingania waingie kwenye wislamu na wala hakumtuma kwenda kupigana .lakini khalid bin Walid akapigana na akauwa baadhi ya watu . Mtume akasema mara mbili : Ewe mwenyezi mungu mimi niko mbali na yale alio yafanya Khalid.
Taz.Sahih bukhar babu bath annabii Khalid bin Walid na babu raful aid fi dua
Musnad Ahmad Juz 2 Uk 150
Mushiklul Aathar Juz 4 Uk 254
Sahih Annasaai babul rad alal hak idha qadhwa bighairil haq
Fatihul bari Juz 8 uk 46
Tarekhul tabar Juz 3 Uk 124
Usudul ghabah Juz 2 Uk 94
Kanzul amal Juz 6 Uk 420.
KHalid bin Walid alimtukana na kumbughudhi na kufanyia uadui Amar(r.a)
Taz. Almustadrak ala sahihain Juz 3 Uk 389
Mushiklul Aathar Juz 4 Uk 255
Musnad Atwaalis Juz 5 Uk 185
Kanzul Amal Juz 1 Uk 242.
Khalid bin Walid alimuuwa Malik bin Nuwairah ambae alikuwa ni muislamu na akamuingilia mke wake .
Taz. Tarekh tabar Juz 2 Uk 502
Tabaqatul kubraa Juz 7 Uk 414
Kwa haya machache katika alioyafanya Swahaba Khalid bin Walid bado anabaki kuwa muadilifu?
Je mtu kuyataja mambo kama hayo ni kuwatukana maswahaba?

Comments