MAULID HUAMBATANA NA KUTEMBELEANA NA KUKIRIMIANA:

MAULID HUAMBATANA NA KUTEMBELEANA NA KUKIRIMIANA:
Bwana Mtume (s.a.w.w.), katika Hadithi zake, ametunasihi tuwe tukifanyiana hayo; na hayo huyapata kwa ukubwa siku za maulidi.
Waislamu wa mtaa mmoja, au mji mmoja, au hata nchi moja -- kwa kuhudhuria sherehe za maulidi ya wenzi wao -- hupata fursa ya kutembeleana na kukirimiana.
Kwa njia hii hujuana hali, wakasaidiana na kupapeana moyo.
Hilo huleta mapenzi na mshikamano baina yao.
Na iwapo pale pasomwapo maulidi Waislamu ni wachache, kutembelewa kwao na ndugu zao wanaotoka sehemu nyengine huwatia moyo, na pia huwafanya wahishimiwe na wale jirani zao wasio Waislamu.
Hii ni tabligh kubwa sana katika Uislamu na bila shaka Allah atatulipa kwa hilo.

Comments