MUGHIRAH AWA GAVANA WA KUFA
Mughirah Ibn Shu’bah, ambaye alikuwa kwa asili ni mwenyeji wa Taaif na ameingia Uislamu katika mwaka wa 5 A.H. alikuwa mlaghai mkubwa, muovu na mwenye kupenda madaraka.
Wakati aliposikia kwamba Mua’wiyah ameandaa kwa ajili ya Ziyaad Ibn Abihi ili aishi Kufah na baadaye achukue ugavana wa Kufah kutoka kwake (Mughirah), upesi sana aliteuwa naibu katika Kufah na akaondoka kwenda Sham kukutana na Mua’wiyah.
Alionyesha matakwa yake ya kuhamishwa Kufah, akimueleza Mua’wiyah:
Alionyesha matakwa yake ya kuhamishwa Kufah, akimueleza Mua’wiyah:
“Kwa vile sasa nimekuwa mtu mzima, nakuomba utenge vijiji vichache vya Qirqisiya chini ya mamlaka yangu, ili mwenyewe niweze kujipumzisha.”
Mua’wiyah alitambua kwamba mmoja wa wapinzani wake, kwa jina la Qais, anaishi Qirqisiya na kama Mughirah angekwenda huko anaweza kuunda umoja naye dhidi ya Mua’wiyah.
“Tunakuhitaji na lazima ubakie Kufah,” alisema Mua’wiyah.
“Tunakuhitaji na lazima ubakie Kufah,” alisema Mua’wiyah.
Mughiraha alikataa ofa hiyo, lakini msisitizo wa Mua’wiyah ulimshawishi na kusalimu amri. Ilikuwa ni usiku wa manane wakati Mughirah aliporudi Kufah. Mara moja aliamuru washirika wake kumtoa Ziyad Ibn Abihi na kumpeleka Sham.
Baada ya muda, Mua’wiyah alimteuwa Sa’id Ibn A’as kama gavana wa Kufa badala ya Mughirah, ambaye alimshawishi Yazid (mtoto wa Mua’wiyah) kwa kumuambia:
“Kwanini Mua’wiyah hafikirii kuhusu wewe? Ni muhimu kwamba akuteue wewe kama mrithi wake na mfalme mteule!”
Yazid aliona rai hiyo kuwa yenye kuvutia kiasi kwamba aliiwasilisha kwa baba yake, Mua’wiyah, pamoja na kuungwa mkono na Mughirah, hatimaye Yazid alitangazwa mrithi wa Mua’wiyah.

Wakati huohuo Mua’wiyah alimteuwa Amr A’as kama gavana wa Misr, ambapo aliiweka Kufah chini ya mtoto wake Abdullah Ibn A’as.
Wakati Mughirah alipolifahamu hili, alimuonya Mua’wiyah, “Kwa kitendo hiki, je, hukujiweka wewe mwenyewe katikati ya midomo ya simba wawili?”
Akiwa amepata maelezo ya ujumbe huu, Mua’wiyah alimuondoa Abdullah kutoka Kufah na mara nyingine akamuweka Mughirah kwenye uongozi wa Kufah.
Hivyo, kwa njama mbili za ujanja (Yazid kuurithi ukhalifa, na hila ya ‘katikati ya midomo ya simba wawili’), Mughirah akawa gavana wa Kufah. Baada ya kutawala kwa muda wa miaka saba na miezi michache, alikufa kwa ugonjwa wa tauni akiwa na umri wa miaka arubaini na tisa.5
Rejea:
Paighambar Wa Yaraan, Jz. 5, uk. 272-275.
Paighambar Wa Yaraan, Jz. 5, uk. 272-275.
Comments
Post a Comment