NABII ISA (A.S) NA MKULIMA

NABII ISA (A.S) NA MKULIMA
Imesimuliwa kwamba wakati fulani, Nabii Isa ibn Maryam (a.s) alikuwa amekaa akimtizama mkulima ambaye kwa kutumia sepeto alikuwa akifanya kazi kwa bidii shambani mwake.
Hapo hapo Nabii Isa alimuomba Mwenyezi Mungu: “Ewe Mola! Muondolee matumaini na matarajio” Ghafla yule mtu alitupa sepeto yake pembeni na akakaa chini kwenye kona.
“Ewe Mola! Mrejeshee matumaini na matarajio yake” Nabii Isa (a.s) alimuomba tena Mwenyezi Mungu. Yule mtu aliinuka kutoka kwenye sehehmu yake, akanyanyua sepeto na akaanza kufanya kazi tena.
Nabii Isa (a.s) alimfuata na akauliza, “Kwa nini ulifanya hivyo?” Mkulima alijibu, “Nilijisemea: ‘Mimi ni mzee ambaye maisha yake yamekaribia mwisho, ni kiasi gani ninataka kufanya kazi na kujitaabisha?” Hivyo nikatupa koleo pembeni na nikakaa chini kwenye kona. Lakini baada ya muda, nilijisemea: “Kwa nini hufanyi kazi? Bado uko hai na unahitaji riziki,” na hivyo nikachukua koleo nikarudi kwenye kazi yangu.”
Rejea:
Namunah-e-Ma’arif, Juz.1, uk. 298, Majmua’e Warran.

Comments