HONGERA RADIO IMAN
Assalaam alaykum.
Ninatoa pongezi kwa redio imani
kwa kutoa uchambuzi ulio sahihi wa mgogoro wa Mashariki ya kati. Siku za nyuma
redio hii ilikuwa ikidai kuwa vita vya mashariki ya kati vinasababishwa na
Mashia. Lakini kwa leo, wameweka wazi, uwazi ambao kama watu watakuwa
wamewaelewa, vita baina ya waislamu vitapungua kama sio kuisha kabisa. Leo hii
wamesema kuwa:
1. Mashia
ni waislamu.
2. Vita
vya mashariki ya kati ni baina ya waislamu kwa maslahi ya makafiri
3. Vita
vya mashariki ya kati ni vya kiuchumi, havina uhusiano na dini yoyote.
4. Wachochezi
wa vita ni nchi za Magharibi na Israel
5. Ushia
na Usunni unatumika na mabeberi ili kutugawa na kututawala tu, si vinginevyo.
6. Saudi
Arabia na washirika wake wametapeliwa kupambana vita vya adui, yaani kumsaidia
adui (mabeberu) dhidi ya adui wao ambaye
ni Muiran. Sababu ya wao kutapeliwa ni ujinga.
7. Waarabu
wanatumika na nchi za Magharibi kupambana vita visivyokwisha vya kimadhehebu
ili kusahaulishwa mgogoro halisi wa waislam na wayahudi (Au waarabu na wazayuni
huko Palestina).
8. Wafaidika
wa vita vya Mashariki ya kati ni waisrael na wamarekani (WAZAYUNI). Waarabu na
waajemi ni wahanga wa ubeberu wa wamagharibi.
Baada ya maelezo haya, tutumie
akili zetu vizuri, tuwe wamoja, na hivyo kuondoa fikra za migawanyo miongoni
mwetu. Hili litavunja njama za maadui za kutuchonganisha. Hili ni funzo wa sote, sio Mashariki ya kati
peke yake. Kwa kutumia uchambuzi huu tupunguza migogo baina ya mashia, baina ya
Masunni, baina waislamu na baina na waislam na wasio kuwa waislamu.
Lakini wamefanya kosa moja, kudai
kuwa Mashia ni maadui wa wasudia. Hii si kweli kwa sababu sisi wote ni
waislamu, hatuwezi kuwa maadui. Qur’an inatuambia kuwa waislamu ni ndugu,
ukisema waislamu ni maadui unatupa mashaka kuwa hata sisi sote sio waislamu.
Comments
Post a Comment