NI NANI MAWAHHABI

NI NANI MAWAHHABI
Mawahhabi au kama wanavyojiita Answari Sunnah au Masalafi ni kikundi ambacho wao wenyewe wanajiita waislamu, lakini kwa hakika wao ni genge lilojiandaa na kusimama imara kabisa kuupiga vita Uislamu kwa hali na mali na kuvunja hadhi na heshima ya Mtume wetu, ikiwa ni pamoja na kuwatukana, kuwakashfu Maimamu na kuzipondaponda jitihada zao sahihi.
Madhehebu ya Uwahhabi tokea yalipoanzishwa mwaka 1737 miladia mpaka leo yamekuwa ni msingi imara wa kutia chokochoko, fitna na farka miongoni mwa waislamu watulivu kila mahali duniani. Madhehebu yenyewe ni ya uzushi na lengo lake ni kueneza upotovu. Na jambo la ajabu ni kuwa hakuna siku hata moja ambapo Mawahhabi wamejishughulisha na umoja wa waislamu, bali kazi zao ni kuupinga umoja na utangamano.
Matoleo yao yote ya vitabu yanayogharamiwa na fedha za serikali ya Saudi Arabia yanajihusisha zaidi na kukashfu madhehebu ya waislamu wengine na kudai kuwa ni upotovu na ushirikina na kwamba hakuna Uislamu safi isipokuwa uwahhabi ambao umefundishwa na Mohammad Abdulwahhabi, sheikh wa Najdi na kusimamiwa kwa nguvu za dola ya Uingereza na ufalme wa Najdi, kikundi ambacho kiliukubali Utume wa uongo wa Masailama al-Kadhab. Mawahhabi wamewafanya waislamu wengine wote kuwa ni maadui zao, na wakati huo huo serikali yao ya Saudi Arabia imewakumbatia maadui wa Uislamu duniani, kama Marekani, Uingereza na Israel kwa mapenzi na utii.
Hakuna nchi, mji au kijiji chochote ambacho waislamu wamekuwa na umoja toka zamani, isipokuwa mawahhabi waliwasambaratisha maadam tu mhubiri wa kiwahhabi ameingia katika eneo hilo. Kundi la Mawahhabi ni mfano mbaya wa makundi ya kiimani lisilokuwa na uvumilivu wa imani ya waislamu wa madhehebu mengine sembuse wasiokuwa waislamu.
Wahubiri wao si tu kwamba wamepatiwa mafunzo ya kutosha kuwababaisha watu wenye elimu ya chini na kuwapandikiza chuki mbaya dhidi ya waislamu wenziwe. Je kwa nini serikali ya Saudi Arabia inatumia fedha nyingi kuwalipa watu wanaokuja kuwafarakisha watu?
Natazamia kuwa kila mwislamu atajitahidi kuwatahadharisha waislamu wenzetu hasa watoto wajifunze Uislamu sahihi na waepuke fitina za mawahhabi.

Comments