UPOTOSHAJI WA DHANA YA EVOLUTION

UPOTOSHAJI WA DHANA YA EVOLUTION

Baadhi ya wanasayansi kwa kupotoshwa au kutoujua vyema Ukristo walianzisha dhana nyingi kuhusu asili ya dunia na viumbe vilivyomo.

Nadharia hizi za Kikafiri na Sayansi za Karl Marx pamoja na makafiri wote kwa ujumla, hudai kuwa nadharia zao ni zao la magunduzi ya kisayansi. Lakini ukizichunguza nadharia zao si za kisayansi bali ni maelezo ya watu waliochanganyikiwa. Marx mwenyewe na rafiki yake Engels waliitathmini na kuitumia nadharia ya Darwin ya “Evolution”.

Marx na Engels waliiangalia dhana ya chanzo cha mwanaadamu aliyoibuni Darwin kama ni upembuzi wa kiyakinifu (Dialectical-materialist) katika chanzo chake. Hata hivyo wanasisitiza kusema kuwa Darwin mwenyewe hakuwa na habari na dhana hiyo (kuwa yeye ni Mpembuzi - dialectician).

Hivyo basi Marx na Lenin katika mafundisho yao hawakuegemeza tu katika mafanikio ya elimu ya jamii na mafunzo ya kihistoria bali pia waliegemeza katika uvumbuzi wa elimu ya kimaumbile ya wakati wao. Uvumbuzi huu ndio uliokuja kuzaa falsafa ya kisayansi ijulikanayo kama “dialectical and historical materialism” (uyakinifu wa kihistoria na kipembuzi).

Lakini je, wagunduzi wa zama hizo kama Darwin walikuwa wanasayansi kweli? Sayansi ya leo inasemaje juu ya ugunduzi wao?

Ukafiri si Zao la Sayansi. Yawezekana kabisa kina Darwin walikuwa wanasayansi wakubwa katika zama zao. Lakini jambo la hakika ni kuwa hawakufahamu kabisa juu ya uhai na hivyo hawakutumia nadharia za kisayansi katika kuelezea chanzo cha uhai. Bali walitumia njia iitwayo “Naturalistic point of view”.(Nadharia ya kimaumbile).

Darwin na wenzake katika moja ya vikao vyao wanakiri kutofahamu uhakika wa uhai katika maeneo yafuatayo: “The Scientist’s approach to the origin of life is not in need of an exhaustive definition of what life is. We must attack from the naturalistic point of view, namely, that principles unknown or unknowable to science can not be used to solve the problem. In other words, we proceed under the assumption that life is a process that escapes at present our complete understanding only for reasons of its complexity”.

Tafsiri:
“Mtazamo wa kisayansi juu ya chanzo cha uhai hauhitaji
kujiuliza uhai (maisha) ni nini. Hatuna budi kuangalia
nadharia za kimaumbile. Misingi yote isiyotambulika
kisayansi haiwezi kujibu suala hili. Hivyo ni lazima tufahamu
kuwa tunaondokea na dhana kuwa uhai (maisha) uko mbali
na ufahamu wa binaadamu katika maisha ya leo.”

Maelezo haya ya Darwin na wenzake yapo wazi – kwamba nadharia zao wamezijenga juu ya dhana tu na kwamba hawaelewi hakika ya uhai kwa sababu ya utata wake. Bila shaka mwenye akili timamu hawezi kuikubali nadharia iliyojengwa juu ya dhana na si hivyo tu, bali dhana ya mtu asiyeelewa hakika ya kitu anachokitolea nadharia.

Jambo la kushangaza zaidi ni kule kuona jinsi makafiri
wanavyoing’ang’ania dhana ya Darwin na kuiita ya Kisayansi, wakati Darwin mwenyewe anakiri kuwa nadharia yake ya ‘evolution’ ni imani tu ambayo hata yeye mwenyewe hawezi kuithibitisha.

Kwa maneno yake Darwin anasema: “Lakini naamini mabadiliko ya kimaumbile, sio kwamba naweza kuthibitisha angalau jamii moja kwamba imebadilika kutoka hali moja hadi nyingine, ila kwa sababu yanagawanya na kueleza vizuri (kama nionavyo mimi) ukweli wa mambo juu ya mgawanyo wa aina mbali mbali, taaluma ya ufanyikaji na ukuaji wa mtoto tumboni (embryology), ufanyikaji na mgawanyiko wa miti na wanyama, viungo chipukizi, mabadiliko ya udongo na mgawanyiko wake.”

Bila shaka maelezo haya ya Darwin mwenyewe yathibitisha wazi jinsi nadharia ya ‘evolution’ isivyokuwa ya kisayansi. Kwa hivyo basi mtizamo wa makafiri juu ya chanzo cha uhai na mwanaadamu kwamba hakuna muumba, bali ni zao la “evolution” ni imani potofu isiyo na misingi ya kisayansi.

Labda ingekuwa vyema pia kuonyesha hapa kuwa, hata hao
wanasayansi walioiendeleza dhana ya Darwin ya ‘evolution’ wamekiri kuwa inaudhaifu mkubwa kwa sababu inashindwa kujibu maswali mengi ya msingi. Bwana Harlay Shapley katika makala yake “On the Evidences of inorganic evolution”, ana haya ya kusema:-
“Sababu yetu nzito ni kusema kuwa dunia nzima iliibuka kama
ilivyo, lakini namna ilivyoibuka, kutoka wapi na wapi inapoelekea,
ni miongoni mwa masuala tusiyoyajua”.

Nadharia ambayo inashindwa kujibu maswali hayo ya msingi ni
dhahiri kuwa haiwezi kutupa jibu sahihi juu ya chanzo cha uhai,
mwanadamu na lengo la kuumbwa kwake.

Swali la kujiuliza hapa ni kuwa inakuwaje makafiri kuichukua dhana ambayo udhaifu wake umeshadhihirishwa si tu na waasisi wake bali hata na dhana yenyewe?

Tumeona kwenye kurasa za nyuma kuwa Karl Marx alikuwa
miongoni mwa wanafalsafa wa karne ya 19 waliokuwa na chuki kali dhidi ya Ukristo (dini). Kwa hiyo alikuwa tayari kutumia silaha yoyote kutokomezea mbali dini. Kinachofanywa na watu hawa ni kuukomoa ukristo na kwa kufanya hivyo, wanazikomoa dini zote. 

Comments