BAHLUL NA KISA CHA KUJENGA MSIKITI
Fadhil ibn Rabii aliujenga Msikiti katika mji wa Baghdad. Ilipofika siku ya
kubandika kibao, aliulizwa kitu gani kiandikwe juu yake. Naye alishauri kuwa
jina lake liandikwe kwani yeye ndiye aliyeugharamia ujenzi wake. Wakati hayo
yalipokuwa yakitokea, Bahlul pia alikuwapo hapo, naye hakusita kumwuliza:
"Je umejenga msikiti huu kwa ajili ya nani?"
Fadhil alijibu: "Kwa ajili ya Allah (s.w)".

Bahlul alisema: "Iwapo ni kwa ajili ya Allah (s.w) basi usiandikishe
jina lako."
Kwa hiyo, Fadhil alikasirika na akatamka: "Kwa nini nisibandike jina langu? Je watu watamjuaje mtu aliyejenga?"
"Je kwa nini usiandike jina langu?" Akasema Bahlul.

"Loh! Hayo kamwe hayawezi kuandikwa." akamjibu Fadhil.
"Iwapo umejenga huu Msikisti kwa ajili ya kujionyesha na kujifaharisha, basi utambue wazi kuwa thawabu zako kwa Allah (s.w) zimepotea." Hayo ndiyo aliyoyasema Bahlul.
Kwa hayo, Fadhil aliaibika na akanyamaza na kusema: "Fuateni lile alisemalo Bahlul."
Hapo Bahlul akawaambia "andikeni Aya moja ya Quran tukufu na kuitundika mlangoni mwa Msikiti."

NB.
1. Je wapenda sifa kama Fadhil wapo katika jamii zetu au hawapo?
Nina uhakika kuwa wapo, basi
wamwogope Allah ili juhudi na sadaka zao zisijepotea pore.
Comments
Post a Comment