JE KUFUNGA MIKONO KATIKA SWALA NI WAJIBU AU SUNNAH AU NI BID’A ?

JE KUFUNGA MIKONO KATIKA SWALA NI WAJIBU AU SUNNAH AU NI BID’A ?

Wanazuoni wa Ahlul-sunna wamekhitilafiana katika suala hili. kuna baadhi yao wamesema inajuzu na wengine wakasema ni Mustahabu. Ni kauli mbili tofauti, anayesema inajuzu kauli yake inatofautiana na ya yule anayesema ni mustahabu, hilo liko wazi.
kwa Mfano: Maliki amesema "Inajuzu kunyoosha", lakini Mustahabu ni kuachia mikono katika swala ya faradhi". Hambali, Shafii na Hanafi wao wakasema kufunga mikono katika swala ni mustahabu, lakini wakatofautiana sehemu ya kuiweka mikono hiyo.

Hanafi akasema ni sunna kwa mwanaume aweke mikono yake baada ya kufunga chini ya kitovu chake, na mwanamke aiweke kwenye kifua chake.

Shafii akasema: Ni sunna kwa mwanaume na mwanamke baada ya kufunga mikono waiweke chini ya kifua na juu ya kitovu.

Ama Hambali yeye anasema jambo hilo ni sunna na bora zaidi baada ya kufunga mikono basi iwekwe chini ya kitovu.

Pia wote kwa ujumla wamekubaliana na kuafikiana kuwa kufunga mikono katika Swala sio Wajibu. Hakuna mwanazuoni hata mmoja anayesema jambo hilo ni Wajibu katika swala.

Hivyo tutabaki na mjadala kuwa kufunga mikono ni Sunnah au bid’a ? Kama ni bid’a mikono iwekweje ? Kwani Mtume alisali vipi ?

Comments