KUNYOOSHA MIKONO KATIKA SWALA NI WAJIBU
Kwa mujibu wa Madh-hebu ya Ahlul-bayt (a.s) ya "Shia Ithna Ashariya" wenye kuwafuaata Maimamu kumi na wawili (12) (a.s) walioteuliwa na Mtume (s.a.w.w) kuwa Makhalifa wake baada yake, kufunga mikono si SUNNA bali ni BID'A ILIYOWAZI, kwani limeingizwa katika Uislaam baada ya Mtume (s.a.w.w) na kunasibishwa kwake kwa hadithi za uongo na dhaifu kama hizo zilizotajwa na site ya (alhidaaya.com).
Kuna riwaya zimepokelewa na makundi yote mawili (yaani Shia na Ahlus-sunna) zinazothibitisha kuwa swala sahihi ya Mtume (s.a.w.w) haikuwa kwa kufunga mikono si tumboni kwenye kitovu au juu ya kitovu au katika katika ya kifuna na kitovu wala karibu na shingo, bali swala sahihi aliyoiswali aliiswali kwa kunyoosha (kuachia) mikono yake.
Post ijayo nitataja hadithi mbili, insha Allah, moja imepokelewa na (Shia na Ahlus-sunna) na ya pili imepokelewa kwa njia ya Shia Ithna ashariya (Imamiyya) tu.Kupitia hadithi hizi mbili tutakuwa tumethibitisha kuwa Kufunga mikono katika swala ni Bid'a na si Sunna kama wachache walivyodhani.
Comments
Post a Comment