Waislamu husoma maulidi kwa sababu mbalimbali. Kati ya hizo ni:
(i) kuikumbuka na kuitukuza siku aliyozaliwa mbora wa viumbe vyote, aliyetutoa vizani na kututia kwenye nuru;
(ii) ni njia moja ya kutoa shukrani zetu kwa neema hiyo;
(iii) katika sherehe hizo, hupatikana fursa ya kukumbushana maisha ya bwana mkubwa huyo na mafunzo yake;
(iv) hupatikana fursa ya Waislamu wa madhehabi na mataifa mbalimbali kushirikiana na kuziweka kando hitilafu zao; na
(v) mikusanyiko hiyo huleta athari kwa wasio Waislamu ya kuupenda Uislamu, na hata kusilimu.
Comments
Post a Comment