Assalaam alaykum;
Asili ya Jina Shia ni Mtume mwenyewe, pale ambapo mara kwa mara
alikuwa akiwaashiria wafuasi wa Ali kama Mashi‘a.
Mwislamu anapokuwa amebobea katika Uislamu wake ndipo
hujiongeza na kuwa Mshia. Kwa Lugha nyingine Ushia ni Uislamu ulikokomaa, kama ambavyo uwahhabi au usalafi ukikomaa huwa ugaidi chinjachinja.
Hadithi zifuatazo
zinanukuliwa kutoka rejea za Kisunni:- Ibn ‘Asakir anasimulia kutoka kwa
Jabir bin Abdullah kwamba alisema:
“Tulikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipokuja (hapo tulipokuwa). Mtume (s.a.w.w.) akasema:
‘Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo
mikononi mwake, hakika huyu (Ali) na Shi‘a wake ndio wenye kufuzu siku ya
ufufuo.’
Kisha Aya ifuatayo ikashushwa. “Hakika wale walioamini na kutenda mema, basi
hao ndio wema wa viumbe. (Qur’ani 98:7)”
At-Tabarani anasema kwamba, Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali:
“Ewe Ali! Hakika utakuja mbele ya Allah, wewe na Shi‘a wako hali ya kuwa
mmeridhiwa (na Allah) na hali ya kuwa mnaridhia kwa Allah.”
Kuna hadithi nyingi kutoka kwa wasimuliaji wengi ambazo wanachuoni wa Kisunni wasingeweza kuzipuuza.
Hivyo walijaribu kuzifanya hadithi hizi zioane na upande wao. Kwa mfano baada ya kunukuu hadithi hizi, Ibn
Hajar al-Makki anaandika hivi: “Na Shi‘a wa Ahlul Bayt ni Ahlu’s-Sunnah
wa’l-Jamaa (yaani Sunni) kwa sababu ni wao waliowapenda Ahlul Baty kama
ilivyoamrishwa na Allah na Mtume wake. Ama wengine, basi wao ni maadui (wa
Ahlul bayt).”
Dai hili lilirudiwa tena na Shah Abdu ’l Aziz Dehlawi
ambaye anasema: “Ni lazima ieleweke kwamba
Shi‘a wa kwanza (ambao ni Sunni na Tafadhiliyya) katika siku za zamani
walijulikana kama Mashi‘a.Wakati Ghulat na Rawafidh, Zaydiyyah na
Ismailiyyah walipochukuwa jina hili kuwa
lao...... kwa hivyo wakajichukulia jina
la Ahlu ’s-Sunnah wa’l-Jamaa.”
Ingelikuwa masunni
walikuwa wakiitwa Shi‘a, basi angalau baadhi ya viongozi wa Kisunni wangelijulikana kwa jina hili kabla ya kuja
kwa Zaydiyyah (120 A.H.). Aidha, kama Sunni wangelijulikana kwa jina hili,
Zaidiyyah na Ismailiyyah, wasingeweza
kulivumilia jina hili kuwa lao na wangejichagulia jina lingine, haiwezekani mtu
achukue jina la adui yake.”
As-Suyuti, Jalalu’d-Din (aliyekufa 910/1504 – 05) katika
Tafsiri yake ad-Durrul- Manthur, J. 6 uk. 379. Anasimulia hadithi hii kutoka
kwa Ibn Abbas na Ali kadhalika katika
sehemu hiyo hiyo; Al-Khuwarizmi (aliyekufa 569/1173-4) katika al-Manaqib. Hawa
wameeleza wazi ubora wa Mashia wa imam Ally mbele za Allah na Mtume wake.
Hadithi nyingine za Mtume (s.a.w.w.) zitamkazo kwamba Shi‘a
wa Ali watafuzu siku ya kiyama
zinasimuliwa na Wanachuoni wa Kisunni kutoka kwa Abdullah, Abu Rafi,
Jabir bin Abdullah, Ibn Abbas na Ali; Mingoni mwa wanachuoni hawa ni
at-Tabarani katika kitabu chake al-Mu‘jam al-Kabir, Ahmad bin Hanbal
katika al-Manaqib yake, Ibn Mardawayh
al-Kanji ash-Shafi’i katika kitabu chake Kifayatu ’t-Talib na wengine wengi.
Ibn Athir katika an-Nihayah na Ibn Hajar al-Makki katika
as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah (Misri, uk. 92) wanasimulia hadithi nyingi kuhusu suala
hili.
Comments
Post a Comment