MAULIDI HUONYESHA UMOJA NA MSHIKAMANO BAINA YA WAISLAMU

Assalaam alaykum:

Qur'ani Tukufu (Sura 3:103) inatuhimiza tushikamane na tusifarikiane.

Na Mtume naye (s.a.w.w.) anatuhakikishia, katika Hadithi zake, kwamba popote ambapo tutajumuika kwa kheri -- na maulidi ni jambo la kheri -- basi Malaika watatuzunguka, rehema za Mwenyezi Mungu zitufunike, na utulivu wa nyoyo utushukie.

Jee, tunapokusanyika maulidini, hatuyaoni hayo? Ule umoja na mshikamano unaopatikana maulidini, wa wafuasi wa madhehabi mbalimbali kusahau hitilafu zao na kuwa kitu kimoja, ni rehema ndogo?

Hivi hawa watu wanaohubiri mifarakano na mitengano ni sehemu ya waislamu au ni maadui wanaojifanya waislamu ili watupotoshe? Kwa hakika wapenda mifarakano si miongoni mwa waislamu bali wanaigiza tu.

Comments