Kitabu cha Isaya
(28:9-13) kinasema, “Atamfundisha nani maarifa?
Atamfahamisha
nani habari hii? Je! ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Kwa
maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu
ya kanuni, huku kidogo na huku kidogo.
La, bali kwa
midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa; ambao
aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika;
lakini hawakutaka kusikia. “Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi,
amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;
huku kidogo na huku kidogo, ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na
kunaswa, na kuchukuliwa”.
Walioachishwa
maziwa ni wana wa Ismaili ambao waliakhirishwa kupata ujumbe wa Mungu.
Kur’an
tukufu iliteremshwa pole pole, amri juu ya amri, kama ielezavyo bishara hiyo.
Baadhi ya sura zilishuka Makka na nyingine Madina (Huku
kidogo na
huku kidogo).
Kurani
tukufu iliteremshwa katika lugha ya Kiarabu ambayo ni “Midomo ya watu wageni na
lugha nyingine” kwa wana wa Israeli.
Awali
imeelezwa ya kwamba Mtume (s.a.w.w) atakimbilia Madina kwenye raha, mapumziko
na maburudiko, lakini watu wa Makka watazidi kukataa ujumbe wa Uislamu mpaka
watashindwa, kuvunjwa na kunaswa, na kuchukuliwa.
Utabiri huu
uko wazi sana, atakayebisha ameamua tu kuleta ubishi. Nakuombe acheni ubishi na
kujiunga na dini hii takatifu iliyoletwa na mtume huyu wa Mwenyezi Mungu.
Nadhani kila mtu anajua kuwa dini ililengwa katika ujumbe huu ni Uislamu peka
yake.
Comments
Post a Comment