BAADHI YA MASHEIKH WA KISUNNI WAJUA HAKI YA IMAM HUSSEIN JUU YA YAZID {MUUAJI MKUU}.

BAADHI YA MASHEIKH WA KISUNNI WAJUA HAKI YA IMAM HUSSEIN JUU YA YAZID {MUUAJI MKUU}.

Waislamu wasio Shia, hasa wale wa madhehebu ya Hanafii na Shafii wote, na wengi wa Hambali (Wafuasi wa Imamu Ahmad Ibn Hambal) wanamtambua Imamu Husayn (a.s) kuwa na haki na Yazid kuwa yu mwenye makosa.
Wao huungana na Mashia kuomboleza kifo cha imam Hussein na hupingana na Mawahhabi na Masalafi ambao wanafurahia kifo cha Imam huyo mtukufu.
Kuzitaja rejea zote hapa kutaifanya orodha hiyo kuwa ndefu sana. Hivyo nitazitaja baadhi tu ya rejea hizo, nilizozichagua miongoni mwa waandishi walioandika juu ya jambo hili:
1. Allamah Shahabuddin Abul Abbas Ahmad bin Muhammad Qastalani, aliyefariki kwenye mwaka wa 923 Hijiria, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Irshad Alsari Sharh Sahih Bukhari", Juzuu 2, ukurasa wa 139.
2. Bwana Ibn Jawzi (aliyefariki mnamo mwaka 1200 Masihiya), mwenye kitabu chake kiitwacho: "Al-Radd Alal Mutaassib Alanidil Man 'Min Dhulm Yazid."
3. Bwana Sibt Ibn Jawzi (aliyefariki mnamo mwaka wa 1257 Masihiya), mwenye kitabu chake kiitwacho: "Tazkiratu Khawassil Ummam".
4. Allama Ibn Hajar Al-Haitami (aliyefariki mnamo mwaka wa 974 Hijiriya), mwenye kitabu chake kiitwacho: As-Sawa'iq al-Muhriqah, ukurasa wa 132-134.
5. Imamu Jalaluddin Abdul-Rahman Ibn Abi Bakr Al-Suyuti (aliyefariki mnamo mwaka 911 Hijiriya), mwenye kitabu chake kiitwacho: "Tarikhul Khulafaa".
6. Shaikh Muhammad bin Ali Sabban (aliyefariki mnamo mwaka 1792 Masihiya), mwenye kitabu chake kiitwacho: "Is'afur Raghbiin".
7. Allama Sa'duddin Mas'ud bin 'Umar Taftazani (aliyefariki mnamo mwaka 1389 Masihiya), mwenye kitabu chake kiitwacho: "Sharh Aqaid Nasafi".
8. Shah Abdulaziz Dehlawi (aliyefariki mnamo mwaka 1824 Masihiya) mwenye kitabu chake kiitwacho "Sirrul Shahadatain".
9. Shah Abdulhaqq Dehlawi (aliyefariki mnamo mwaka 1642 Masihiya), mwenye vitabu vyake "Mada-rijun Nubuwwat" na "Ja-adhbul Qulub".
10. Maulana Abdulhai Firangi Mahali, mwenye kitabu chake kiitwacho "Fatawi," Juzuu 3, ukurasa wa 7.
11. Nawwab Siddiq Hassan Khan Bhopali (aliyefariki mnamo mwaka 1889 Masihiya), mwenye kitabu chake kiitwacho: "Bughyatul Raid Fi Sharhil Aqaid".
12. Maulana Muhammad Matin Firangi Mahali, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Wasilatun Najat", ukurasa wa 290.
13. Mufti Muhammad Akramuddin, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Sa'adatun Kawnain Fi Fadhailil Hassanain."
14. Qadhi Muhammad Sulaiman, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Rahmatuh-Lil- 'Alamiin".
Majina haya machache ni mifano michache tu yenye kuwajumlisha wanachuoni wa kihanafiyah, Kishafi'i na Kihambaliya ambao wameweka sehemu ya Imamu Husayn kuwa ilikuwa ya haki na kwamba alikufa akiwa shahidi aliyedhulumiwa.
Kinyume na hivyo, wako Mahambaliya wanaoamini kuwa Ibn Taimiya ni kiongozi wao; na hivyo ndivyo waaminivyo Nasibi, Salafi swaleh, wahhabi, Answari Sunna na Kharji, ambao ili kuwahadaa Masunni, hujitokeza kama Masunni. Watu hawa humchukulia Yazid kuwa ni khalifa wa kweli na hivyo, Mwenyezi Mungu na atusamehe, humchukulia Imamu Husayn (a.s) kuwa yu mwenye makosa aliyestahili kuuawa.
Siku hizi, maoni ya namna hii yanatolewa na Mahmud Ahmad Abbasi, ambaye kitabu chake kiitwacho "Khilafat Muawiya wa Yazid" kimeziumiza hisia za Waislamu wengi. Kwenye siku za awali, kabla ya Ibn Taimiya (aliyefariki mnamo mwaka 728 Hijiriya), mtu mmoja aliyeitwa Abu Bakr Muhammad bin Abdullah bin al-Arabi (aliyefariki mnamo mwaka 543 Hijiriya) alijitokeza kwenye itikadi hiyo hiyo. Mtu huyo aliandika hivi: "Husayn hakuuawa ila kwa upanga wa babu yake mwenyewe (yaani kwa mujibu wa kanuni za shari'ah), kwa sababu kililiwa kiapo cha utii kwa Yazid na hivyo Husayn alikuwa mwasi".
Maelezo ya huba yake kwa Yazid yaliyomo kwenye kitabu kiitwacho "Tazkiratul Huffaz".: "Hafidh, Allama, Qadhi, Faqihi, alifikia daraja la Ijtihad". Abu Bakr bin Al-Arabi alikuwa mwanafunzi wa Imamu Ghazali (aliyefariki mnamo mwaka 505 Hijiriya). Imamu Ghazali huyu ndie yule yule aliye maarufu kwa jina la Hujjatul Islam na anaaminiwa kuwa yu nguzo ya kanuni za kidini (za Kisunni) na mmoja wa wale ambao Fat'wa (hukumu ya Kiislamu) zao zilikuwa: "Ni haramu kuhadithia juu ya Husayn na wafuasi wake kwenye hotuba, kwa sababu kufanya hivyo kunazaa chuki juu ya masahaba". Ni dhahiri kwamba, kama Imamu Ghazali aliifikiria sehemu ya Imamu Husayn (a.s) kuwa ni ya haki, asingeharimisha kuihadithia. Tukiyafikiria yote haya, mtu hatakuwa na jingine la kufanya ila kuamua kuwa, Ulama kama hawa hawamfikirii Imamu Husayn (a.s) kuwa yu mtu mtukufu na kwamba, kwa mujibu wa maoni yao, kukataa kwa Imamu Husayn (a.s) kula kiapo cha utii kwa Yazid kulikuwa ni kosa kubwa mno kiasi kwamba hadi hivi leo wanaandika kuwa, Mwenyezi Mungu na atusamehe Imamu (a.s) alikuwa na dalili za ukaidi.
Hii ni dhahili kuwa Mawahhabi, masalafi, Answari Sunnah na wengineo wenye misimamo kama yao ndio wauaji wa Imam Hussein na ndio sababu ya wao kufurahia mauaji hayo. Allah awalaani wauaji wa imamu wetu huyu

Comments