MASHIA NDIO WAISLAMU SAHIHI
Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i, mmoja wa wanachuo mashuhuri wa Sunni katika kitabu chake “Mawaddatul’l-Qurba” na mwanachuo anayejulikana vizuri sana kwa upinzani wake juu ya Shia, Ibn Hajar katika kitabu chake “Sawa’iq-e-Muhriqa”, anasimulia kutoka Ummu’l-Mu’minina Ummu Salama, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwamba Mtume alisema: “Ewe Ali, wewe na Mashia wako mtaishi.”
Mwanachuo anayejulikana sana wa Khawarizm, Muwaffaq bin Ahmad, katika
kitabu chake “Manaqib” Sura ya 19, anasimulia kutoka rejea zinazoaminika kwamba
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali: “Katika umma wangu wewe ni kama Masihi Isa Mwana wa Mariamu.”
kitabu chake “Manaqib” Sura ya 19, anasimulia kutoka rejea zinazoaminika kwamba
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali: “Katika umma wangu wewe ni kama Masihi Isa Mwana wa Mariamu.”
Taarifa hii inaonyesha kwamba, kama vile wafuasi wa Mtume Isa (A.S) walivyogawanyika katika makundi: Waumini wa kweli wajulikanao kama Hawari’in, Mayahudi, na wapiga chuku (wenye kutia maneno chumvi) ambao wanamshirikisha yeye na Allah; katika njia hiyo hiyo Waislamu watakuja kugawanyika katika makundi matatu. Mojawapo litakuwa Shi’a, waumini wa kweli. Kundi lingine litakuwa la maadui wa Ali, na kundi la tatu litakuwa la wenye kukuza cheo chake.
Comments
Post a Comment