MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {V}

MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {V}

{1}Kusameheana:
Mwenyezi Mungu amesema: "Na mkiwasamehe na kupuuza yaliyopita na kuyafuta kabisa katika nyoyo zenu {basi Mwenyezi Mungu} atafurahi kwani Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwingi wa rehema." {Qur'an, Sura ya 64, aya ya 14}.

Hivyo waislamu tunatakiwa tuwe wepesi wa kuwasamehe waliotukosea, hasa pale wanapotuomba msamaha tusithubutu kugoma kuwasamehe, vingine nasi hatutosamehewa na Allah (s.w).

{2}Kukidhi haja za watu:
Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Mwenye kukidhi haja ya nduguye mwenye kuamini {Muislamu} basi kama amefanya ibada ya Mwenyezi Mungu maisha yake."

Waislamu tunahitaji kutoa misaada kwa wahitaji wote bila kujali dini wale upendeleo, japokuwa waislamu wanatakiwa wawekewe mpango maalumu wa kuwainua kiuchumi na kijamii.

{3}Kufanya usawa kwa kila kitu: 
Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Unachopendelea kwa ajili ya nafsi yako, wapendelee wenzio pia. Fanya usawa kati ya wake wako kama unao wengi na kati ya wanao, wala usipendelee kabisa."


Mwenyezi Mungu amesema: Lawama iko juu ya wale wanao dhulumu watu na wakawafanyia jeuri katika ardhi pasipo haki. hao ndio watakao pata adhabu. {Qur'an, Sura ya 42 aya ya 42}

Comments