MFUMO WA JUA (SOLAR SYSTEM)
Kwa mujibu wa taaluma
ya sayansi, Dunia (earth) na sayari
nyingine zinazozunguka
jua, hufanya ulimwengu (universe) ambao kwa vipimo vyetu vya kibinaadamu ni
mkubwa mno.
Dunia (earth) yetu hii
ipo umbali wa kiasi cha maili 93 Milioni kutoka kwenye jua. Umbali huu ni
mkubwa sana kwa mwanaadamu, lakini ni mdogo sana ukilinganishwa na umbali
unaolitenganisha jua na sayari iliyo mbali kuliko zote katika “Solar System”
yetu hii, Pluto. Umbali baina ya jua na Pluto ni mara 40 zaidi ya umbali kati
ya jua na dunia. Yaani kiasi cha maili 3720 Milioni. Pamoja na kuwa mwanga wa
jua husafiri kwa mwendo wa kasi sana – mwendo wa maili 186,000 kwa sekunde,
lakini huchukua takriban saa 6 kwa mwanga huo kufikia Pluto.
Dunia ina umbo la
duara dufu, yaani duara isiyokamilifu mfano wa chungwa, kwa maana kwamba umbali
kutoka ncha ya kaskazini kwenda ncha ya kusini ni mfupi zaidi ya umbali kutoka
mashariki mpaka magharibi kwa katikati ya dunia.
Dunia hulizunguka jua
katika mzunguko ambao waingereza huuita revolution kwa muda wa mwaka mmoja.
Yaani kila mwaka mmoja dunia hukamilisha mzunguko mmoja wa kulizunguka jua.
Mzunguko huu ndio huzaa majira mbali mbali ya mwaka, yaani masika na kiangazi
kwa uchache.
Dunia pia hujizungusha
yenyewe katika mhimili wake. Mzunguko huu waingereza huuita rotation na
huichukua dunia siku moja (saa 24) kukamilisha mzunguko wake mmoja wa
kujizungusha kwenye mhimili wake. Hatima ya mzunguko huu ni kutengeneza usiku
na mchana, kutokana na upande mmoja kuangaziwa na miale ya jua na upande
mwingine kuwa gizani.
Huu ndio ulimwengu
unaomzunguka mwanadamu kama unavyotambulika na wanasayansi.
Comments
Post a Comment