UTABIRI WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) NDANI YA BIBLIA
Siku ya
mkutano katika Horeb, wana wa Israeli walipokataa kusikia sauti ya Mwenyezi
Mungu. Mungu alimwambia Musa. "Wametenda vema kusema walivyosema, mimi
nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia
maneno yangu kinywani mwake. naye atawaambia yote nitakayomwamuru. "Hata
itakuwa, mtu asiyeyasikiliza maneno yangu atakayoyasema yule kwa jina langu,
atauawa. Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo
sikumwagiza kulinena, au atakayenena kwa jina la miungu wengine, nabii yule
atakufa." (Kumbukumbu la Torati 18.16-20).
Utabiri huu mtukufu
unaonyesha mambo haya yafuatayo.
(i) Wana wa
Israeli hawatasikia tena sauti yenye nguvu ya Mwenyezi Mungu.
(ii)
Anayebashiriwa kufika ni Nabii.
(ill)
Ataondokeshwa miongoni mwa ndugu wa Waisraeli.
(iv) Atakuwa
mfano wa Musa.
(v) Maneno
atakayoyasema yatakuwa ufunuo wa Mungu.
(vi)
Atawaambia yote atakayoambiwa na Mungu.
(vii)
Atanena hayo kwa jina la Mungu.
(viii)
Asiyetaka kusikia maneno hayo ataadhibiwa.
(ix) Nabii
wa uwongo atakayesingizia kutumwa na Mungu
atauawa.
(x)
Atakayesema kwa jina la miungu wengine atauawa.
Sasa ni watu
wawili wanaosemwa kuwa wametabiriwa katika Utabiri huu. Wakristo wanasema ni
Yesu, na Waislamu tunasema ni Muhammad (s.a.w.w). utabiri wenyewe hautaji jina
la mtu ye yote, ila tu imeeleza alama kumi za Nabii huyo.
Basi tuzichunguze
alama hizo zinamwangukia nani katika manabii hawa wawili.
(i) Katika utabiri
huu Waisraeli wanaambiwa kwamba hawatasikia tena sauti ya Mungu. Na inajulikana
pote ya kuwa Yesu alikuwa Mwisraeli aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi (Mathayo.
Mtume
Muhammad (s.a.w.w) alikuwa Mwarabu. Hakuwa katika kizazi cha Waisraeli
kilichonyimwa baraka za Mungu, kwa kukataa kwao kusikia sauti ya Mungu.
(ii) utabiri
huu unasema huyo anayebashiriwa kufika ni nabii. Wakristo wanaamini ya kwamba
Yesu alikuwa “Mungu-Mwana” au Mungu Mwenyewe, nao hawataki kabisa Yesu aitwe
nabii. Lakini Mtume (s.a.w.w) aliitwa Rasuulullaahi (Mtume wa Mungu) na pia Nabiyyullaahi (Nabii wa Mungu).
(iii)
lkumbukwe kwamba nabii Ibrahim - baba wa manabii – ndiye aliyemzaa Ismaeli na
Isihaka. Wazao wa Ismaeli ndio Waarabu, na wazao wa Isihaka ndio Waisraeli.
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alitokana na Waismaeli ambao ni ndugu wa Waisraeli,
kama inavyoagua bishara hiyo. Lakini Yesu mwenyewe ni Mwisraeli, wala hakutoka
katika ndugu wa Waisraeli. Hivyo utabiri huu si wake.
(iv) utabiri
unaeleza tena ya kuwa mtume huyo atakuwa mfano wa Musa. Nasi tunaona ya kuwa
Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndiye anayeitwa mfano wa Musa katika Kurani tukufu (73:16).
Yesu angewezaje kujifanya kama Musa hali mwenyewe alikuwa chini ya Sheria ya
Musa? (Mathayo 5:17, 7:12, Marko 10:19. Matendo 24:14).
Hali ya
Mtume Muhammad (s.a.w.w) na ya Nabii Musa (a.s) zinafanana sana. Nabii Musa
alizaliwa na wazazi wawili wala hakulaumiwa katika kuzaliwa kwake. Tena Musa
alioa, alipewa Sheria mpya, alihama nchi yake baada ya kupewa utume, alipigana na
adui zake, nao wakaangamia mbele ya macho yake, alikufa kifo cha kawaida,
walitokea maimamu na mawalii katika umati wake, na mwishowe alikuja Masihi
kusimamisha Sheria ya Musa.
Hayo yote
yalipatikana kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na hivyo
wamefanana
kabisa. Sheria ya Mtume Muhammad itasimishwa tena hapa duniani pindi
atakaporudi imam Mahdi (a.s). Lakini hakuna hata alama moja ya hizo inayopatikana
katika dhati ya Yesu (a.s) sawa na itikadi za Wakristo.
(v) utabiri
unaendelea kusema: “Nami nitatia maneno yangu kinywani mwake”. Yaani Mungu
atamteremshia maneno yake.
Alama hii
pia haionekani katika Yesu. Wakristo wanaamini ya kuwa Yesu alikuwa Mungu, kwa
hivyo hakukuwa na haja ya kufunuliwa maneno kutoka kwa Mungu. Zaidi ya hayo,
Kurani ndiyo Sheria ya pekee inayostahili kuitwa “Maneno ya Mungu”, maana haina
hata neno moja lisilotoka kwa Mungu Mwenyezi.
(vi) Mtume (s.a.w.w)
anaambiwa na Mwenyezi Mungu kufikisha yote aliyoteremshiwa (Kurani tukufu
5.68). Yesu (a.s) aliwaambia wanafunzi wake ya kuwa hatawaambia yote (Yohana
16.12-13). Hivyo utabiri huu haumhusu Yesu.
(vii) Alama
ya saba pia haionekani katika Yesu. Mtu anayesoma Injili anajua ya kwamba
Injili yote haina sura iliyoanza kwa jina la Mungu. Yesu anasema mara kwa mara.
“Bali mimi nawaambieni” (Mathayo 5:22. 28, 34. 39. 44). Luka anasema, ameandika
Injili yake kwa sababu. “Nimeona vema mimi nami kwa kuwa nimejitafutia usahihi
wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofile Mtukufu”
(Luka 1:3-4). Hasemi kwamba alifunuliwa na Mungu, au ameongozwa na Roho
Mtakatifu, wala hakuandika Injili hiyo ili watu wote waisome, bali alimwandikia
mtu mmoja tu, Theofile. Paulo alisema. “Kwa habari za wanawali, sina amri ya
Bwana. Lakini natoa shauri langu” (Wakorintho 7:25).
Ni dhahiri
ya kwamba lnjili za leo ni mkusanyiko wa maneno ya watu mbali mbali. Lakini
Kurani inataja jina la Mwenyezi Mungu katika mwanzo wa kila sura, na inaonekana
Mungu alikusudia kutimiza alama hiyo wazi wazi. Tena Mtume (s.a.w.w) kabla ya
kuanza kazi yo yote alikuwa anataja jina la Mwenyezi Mungu.
(viii)
Waliokataa kusikiliza maneno ya Mungu yaliyotoka kinywani
mwa Mtume (s.a.w.w)
na kuanzisha upinzani waliadhibiwa hapa hapa duniani. Vita vikali vilivyoangamiza
maadui wa Uislamu vilikuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyoahidiwa katika utabiri
huu, na bado kuna adhabu ya
akhera
itakayowawakia walio maadui wa haki. Maadui kwa chuki zao za kukataa
kuusikiliza ujumbe wa Mwenyezi Mungu walikusanya majeshi ili kuufutilia mbali
Uislamu. Mwenyezi akawaamuru waislamu wajilinde. Wakapigana kwa msaada wa Allah
wakawashinda maadui wao pamoja na kwamba waislamu walikuwa wachache tena wenye
zana duni kabisa.
(ix)
Wapinzani wa Uislamu wanasema ya kwamba Mtume (s.a.w.w)
alizua
uwongo. Utabiri huu unawajibu na kusema mtu ye yote
atakayemzulia
Mungu atauawa. Mtume (s.a.w.w) alikaa miaka mingi
duniani na
akisha maliza kazi yake akafariki kifo cha kawaida.
Lakini Yesu
je? Tukifuata imani ya Wakristo kuwa aliuawa msalabani, tunashurutishwa kusema
ya kuwa (Mungu apishe mbali) alikuwa mwongo, maana bishara yasema kuwa nabii wa
uwongo ndiye atauawa. Hivyo kufaulu kwa Mtume (s.a.w.w) na maendeleo ya kazi
yake ni dalili zilizo wazi za ukweli wake.
(x) Bishara
inaeleza tena ya kuwa mwenye kusema neno kwa jina la miungu wengine “Nabii yule
atakufa”. Kwa kuwa Mtume (s.a.w.w) hakuuawa basi imethibitika ya kwamba yote
aliyosema alifunuliwa na Mungu.
Muhammad wa aali Muhammad, swalawaatu
Shukran
ReplyDelete